Tag: Yanga FC

  • Suruhisho la mechi ya yanga Vs Simba leo

    Leo, Machi 27, 2025, viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), pamoja na klabu za Simba na Yanga, wanakutana katika ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) chini ya usimamizi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Lengo la kikao hiki ni kujadili hatma ya mechi ya watani wa jadi, maarufu kama Kariakoo Derby, ambayo iliahirishwa tarehe 8 Machi 2025 kutokana na sintofahamu iliyotokea kabla ya mchezo huo. Pande zote zimehakikisha ushiriki wao katika kikao hiki muhimu.

    Kikao cha leo kinatarajiwa kutoa mwongozo kuhusu lini na jinsi gani mechi hiyo itachezwa, pamoja na kujadili masuala mengine muhimu yanayohusu mchezo huo na mustakabali wa soka la Tanzania.

    FOLLOW The Street Media

  • 🚨SERIKALI KUINGILIA KATI MECHI YA DABI

    ➡️Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania , Profesa Palamagamba Kabudi anatarajiwa kukutana na viongozi wa Simba Sports Club na Young Africans kuzungumzia sakata la uamuzi wa Simba kugomea mechi ya watani wa jadi iliyokuwa ifanyike Machi 8, 2025 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

    ➡️Wengine ambao wanatarajiwa kushiriki kikao hicho kilichopangwa kufanyika Machi 27 mwaka huu ni viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na viongozi kutoka bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPBL).

    ➡️Timu ya Simba Sports Club iligomea mchezo huo kwa madai ya ukiukwaji wa Kanuni namba 17(45) ya Kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo inaruhusu timu ngeni kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi angalau mara moja kabla ya siku ya mechi.