Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza rasmi majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya kati kwa mwaka wa masomo 2025. Uteuzi huu ni hatua muhimu kwa wanafunzi wa Kitanzania waliomaliza mtihani wa kidato cha nne.
Kwa mwaka 2025, kati ya wanafunzi 197,426 waliofaulu, wanafunzi 56,801 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya kati, vikiwemo vyuo vinavyotoa stashahada katika fani mbalimbali za ufundi stadi.
Mchakato wa Uchaguzi wa Wanafunzi
Serikali, kupitia TAMISEMI, imeendesha mchakato wa uteuzi kwa kuzingatia:
- Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne: Matokeo haya yanazingatiwa katika upangaji wa nafasi.
- Mapendekezo ya Mwanafunzi: Wanafunzi huorodhesha vyuo wanavyopendelea.
- Upatikanaji wa Nafasi: Wanafunzi wanapangwa kulingana na nafasi zilizopo vyuoni.
- Ufaulu: Wanafunzi wenye alama za juu wanapewa kipaumbele.
- Mazingatio ya Kanda: Usambazaji wa wanafunzi huzingatia kanda kwa usawa.
Jinsi ya Kuangalia Majina
Majina ya waliochaguliwa yanapatikana kwenye tovuti rasmi za TAMISEMI na NACTVET:
- TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz
- NACTVET: www.nactvet.go.tz
- All
- Vyuo vya Kati
- Vvyuo vya uchumi
- Vyuo vya afya
- vyuo vya maendeleo ya jamii
- Vyuo vya kilimo
- vyuo vya dini
- vyuo vya sheria
- Vyuo vya technology
Unaweza pia kuangalia kwa kubofya jina la mkoa uliofanyia mtihani, kisha wilaya na shule yako. Angalia majina katika mikoa ifuatayo:
- ARUSHA
- DAR ES SALAAM
- DODOMA
- na mengineyo…
Usikose kutembelea tovuti hizi kwa taarifa zaidi na maelekezo muhimu.
Comments