JKT PDF JKT PDF! DOWNLOAD.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA POLISI TANZANIA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania anatangaza nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha sita na Kidato cha nne wenye sifa zifuatazo:

1. Sifa za Muombaji

a) Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.

b) Wazazi wake wawe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.

c) Awe amehitimu kidato cha nne au sita kuanzia mwaka 2019 hadi 2024.

d) Kwa waombaji wa kidato cha nne na sita pamoja na wenye Astashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25.

e) Kwa waombaji wa kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la nne (Division I – IV). Kwa waombaji wenye ufaulu wa daraja la nne (Division IV) wawe na ufaulu wa alama (Points) 26 hadi 28.

f) Kwa waombaji wa kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la tatu (Division I – III). g) Wahitimu wa Shahada na Stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30.

h) Awe na urefu usiopungua futi tano na inchi nane (5’8”) kwa wanaume, na futi tano inchi nne (5’4”) kwa wanawake.

i) Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA).

j) Awe na uwezo wa kuongea lugha ya Kiswahili na Kingereza kwa ufasaha.

k) Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.

l) Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto/watoto.

m) Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya za aina yoyote.

n) Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.

o) Awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.

p) Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.

q) Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa kwenye usaili. r) Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).

s) Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.

t) Kwa waombaji wenye elimu ya kiwango cha Shahada (NTA level 8), Stashahada (NTA level 6) na Astashahada (NTA Level 5 au NVA Level 3) wanatakiwa wawe na fani zilizoainishwa kwenye tangazo hili.

2. Utaratibu wa kutuma Maombi

  1. Waombaji wote wanatakiwa waandike barua za maombi wao wenyewe kwa mkono (Handwriting) bila kusahau namba za simu na watumie anuani ya Mkuu wa Jeshi la Polisi S.L.P 961 DODOMA. Barua hiyo iambatishwe kwenye maombi ikiwa kwenye mfumo wa ‘pdf’.
  2. Waombaji wote wafanye maombi yao kupitia kwenye mfumo wa Ajira wa Polisi (TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT PORTAL) unaopatikana kwenye kiunganishi (link) cha tovuti ya Jeshi la Polisi (https://ajira.tpf.go.tz). Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta, barua pepe (email) au kwa mkono hayatapokelewa.
  3. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 04/04/2025.


FANI ZINAZOTAKIWA KWA KILA NGAZI YA ELIMU

TANZANIA BARA

Shahada

  1. Anesthesia
  2. Animal Science
  3. Anthropology
  4. Architecture
  5. Automobile Engineering
  6. Biology
  7. Biomedical Engineering
  8. Biotechnology and Laboratory Science
  9. Botany
  10. Civil Engineering
  11. Computer Engineering
  12. Computer Information System
  13. Computer Network and Security Engineering
  14. Computer Science
  15. Cyber Crime and Cyber Security
  16. Cyber Forensic and Cyber Security
  17. Database Administration
  18. Electrical Engineering
  19. Film and Video Production
  20. French, Portuguese, Chinese and Arabic
  21. General Agriculture
  22. Gynecology
  23. Journalism and Mass Communication
  24. Land Management and Evaluation
  25. Law Enforcement
  26. Marine Engineering
  27. Marine Transportation and Nautical Science
  28. Mechanical Engineering
  29. Medical Doctor
  30. Medical Laboratory
  31. Multimedia Content
  32. Network Engineering
  33. Nursing
  34. Pediatrician
  35. Pharmacy
  36. Physiotherapy
  37. Psychiatric Nurse
  38. Quantity Surveyor
  39. Radiology
  40. Range Management
  41. Real Estate
  42. Records and Archive Management
  43. Shipping and Logistics Management
  44. Sign Language/Special Needs
  45. Software Engineering
  46. Statistics
  47. System Development
  48. Tax Management
  49. Telecommunication and Electronics Engineering
  50. Translation and Interpretation
  51. Veterinary Medicine

Stashahada

  1. Animal Health and Production
  2. Auto Electrical Engineering
  3. Cartography
  4. Clinical Dentistry
  5. Clinical Medicine
  6. Forensic Science
  7. Graphic Design, Multimedia and Animation
  8. Information and Communication Technology
  9. Masterfisherman
  10. Music
  11. Nursing and Midwifery
  12. Optometrist
  13. Performing and Visual Arts
  14. Radar Operation
  15. Sound Engineering
  16. Wildlife Management

Astashahada

  1. Air Conditioning and Refrigeration
  2. Aluminum and Glass Working
  3. Autobody Repair
  4. Aviation Quality Manager
  5. Aviation Safety Manager
  6. Boat Painting
  7. Boat Skippers for Autobody Engineering
  8. Car Interior Design
  9. Car Paint Technician
  10. Carpentry and Joinery
  11. Clearing and Forwarding
  12. Divinity
  13. Drone Operation
  14. Electrical Installation
  15. Excavator Operation
  16. Film Production
  17. Fitter and Turner
  18. Forensic Science
  19. Hydraulic and Pneumatic Mechanics
  20. Industrial Electrical Engineering
  21. Islamic Knowledge
  22. Judo, Karate, Boxing and Taekwondo
  23. Laboratory Technician
  24. Mandatory Courses
  25. Marine Electrical Engineering
  26. Mason and Brick Laying
  27. Medical Records
  28. Motorcycle Mechanics
  29. Motor Rewinding
  30. Motor Vehicle Mechanics
  31. Offset Printing
  32. Paintings and Sign Writing
  33. Performing and Visual Arts
  34. Plumbing and Pipe Fittings
  35. Printing Machine Operation
  36. Radio/Electronics and Communication Technology
  37. Rating Part Engineering
  38. Rating Part Navigation
  39. Scuba Diving
  40. Sewing Machine Maintenance
  41. Tailoring
  42. Truck and Heavy Duty Mechanics
  43. Veterinary Laboratory
  44. Welding and Fabrications

ZANZIBAR

Shahada

  1. Accounting and Finance
  2. Civil Engineering
  3. Computer Science
  4. Electronics and Telecommunication
  5. Geography and Environmental Studies
  6. Insurance and Risk Management
  7. Journalism and Broadcasting
  8. Law/Law Enforcement
  9. Medical Doctor
  10. Medical Laboratory
  11. Multimedia Technology
  12. Nurse
  13. Pharmacy
  14. Procurement and Supply Management
  15. Psychiatrist
  16. Radiology

Stashahada

  1. Animal Health and Production
  2. Civil Engineering
  3. Clinical Medicine
  4. Computer Science
  5. Counselling and Psychology
  6. Electrical Engineering
  7. Electronics and Telecommunication
  8. Hospitality and Tourism Management
  9. Human Resource Management
  10. Information and Communication Technology
  11. Mechanical Engineering
  12. Medical Laboratory
  13. Nursing and Midwifery
  14. Pharmaceutical Science
  15. Physiotherapy
  16. Record and Archives Management
  17. Science with Education
  18. Sign Language

Astashahada

  1. Carpentry and Joinery
  2. Driving
  3. Electrical Installation
  4. Hotel Management
  5. Housekeeping
  6. Mason and Brick Laying
  7. Plumbing and Pipe Fittings
  8. Tailoring

Imetolewa na:

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,

Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,

S.L.P 961,

DODOMA.

20/03/2025.

Categorized in: