JKT PDF JKT PDF! DOWNLOAD.

Hosea mchopa amezungumza na kocha wa Tabora United Anicet Kiazayidi Makiadi @kiazmak ambaye yupo kwenye kozi ya refresh Congo baada ya taarifa za uvumi kuwa amevunjiwa mkataba na timu ya Tabora United ambao wanaotarajiwa kumtangaza rasmi kocha Mpya Mzimbabwe, Genesis Mangombe.
Makiadi amesema mashabiki wake na Tabora United kwanza amewakumbuka sana na ameahidi atarudi kwani hakuna sababu inayomzuia kurudi Tanzania kwa sababu ana mkataba na timu ya Tabora United.
Amesema yupo Tabora United na ataendelea kufundisha kitu ambacho anaamini amekifanya vyema mpaka sasa akiwa Tabora United.
Pia amesifu ukuaji wa Ligi ya Tanzania akijivunia kuwa sehemu ya makocha wanaoshiriki safari hiyo.
Kuhusu wachezaji wa Kitanzania amesifu vipaji vya wachezaji wazawa akiwemo Offen Chikola na kutamani kuona wachezaji wengi wa Kitanzania wakifanya vizuri zaidi.

Categorized in: