MDAs & LGAs
219 Positions
Application Period
18/10/2025 – 01/11/2025
Duties and Responsibilities
i.Kudhibiti na kuzuia milipuko ya magonjwa;
ii.Kupambana na kuzuia wadudu na wanyama wanaoeneza magonjwa;
iii.Kusimamia uzikaji wa maiti zisizotambuliwa na zile zinazotokana na magonjwa ya kuambukiza;
iv.Kuandaa taarifa mbali mbali za Afya ya Mazingira katika ngazi ya kata na kuziwasilisha katika mamlaka husika;
v.Kukusanya na kuchambua takwimu za Afya ya Mazingira, katika kata na kutoa mrejesho ili kuchukua hatua zinazostahili;
vi.Kutoa elimu ya afya ya mazingira kwa jamii;
vii.Kukagua mazingira katika sehemu zinapotengenezwa vyakula ili kuhakikisha usalama na afya ya jamii;
viii.Kusimamia sheria za afya ya mazingira katika ngazi ya Kata pamoja na kusaidia jamii katika kutengeneza sheria ndogondogo;
ix.Kuhamasisha jamii katika kuboresha vyanzo vya maji na Usafi wa Mazingira;
x.Kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa Huduma za Afya ya Msingi katika ngazi ya Kata; na
xi.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
Qualifications
Kuajiriwa wenye Astashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Remuneration
TGHS A