Nyanya ni zao la mboga linalotumika sana duniani kwa matumizi ya nyumbani na biashara. Kwa Tanzania, ni mboga maarufu inayolimwa na kutumika kwa wingi.
Asili ya nyanya ni Amerika ya Kusini, ikianzia Peru au Ecuador. Nchi zinazoongoza kwa kilimo cha nyanya ni USA, Italia, Mexico, na kwa Afrika ni Malawi, Zambia, na Botswana. Tanzania, mikoa kama Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, na Mbeya inaongoza kwa uzalishaji wa nyanya.
Mazingira Yanayofaa kwa Kilimo cha Nyanya
Hali ya Hewa: Nyanya hustawi kwenye joto la nyuzi joto 18-27°C. Mvua nyingi inaweza kusababisha magonjwa kama ukungu.
Udongo: Hustawi kwenye udongo wenye mboji, usiosimamisha maji, na pH ya 6.0 – 7.0.
Mwinuko: Bora kwenye mwinuko wa mita 400-1500 kutoka usawa wa bahari.
Mbegu Bora za Nyanya
Nyanya Ndefu (Indeterminate): Kama ANNA F1 na Tengeru 97. Zinapendelea kilimo cha greenhouse na zina mavuno ya muda mrefu.
Nyanya Fupi (Determinate): Kama Tanya na Roma VF, nzuri kwa kilimo cha kawaida.
Kulingana na Uchavushaji: OPV (Open Pollinated Variety) na Hybrid. Hybrid zinatoa mavuno mengi na ni sugu kwa magonjwa.
Maandalizi ya Shamba
Andaa shamba mwezi kabla ya kupanda.
Tumia mbolea kama samadi na DAP wakati wa kupanda.
Nafasi kati ya miche ni sentimita 50 – 60 kwa 50 – 75.
Ondoa magugu mara kwa mara ili kuzuia ushindani wa virutubisho na magonjwa.
Mahitaji ya Mbolea
Mbolea za Kupandia: DAP au Minjingu.
Mbolea za Kukuzia: CAN, NPK, au SA kila baada ya wiki mbili tatu.
Kuweka Matandazo
Tumia nylon au majani ya migomba kuboresha unyevu na kuzuia magugu.
Kupogolea Matawi na Majani
Punguza matawi na majani yasiyo na msaada ili kuruhusu mzunguko wa hewa.
Changamoto za Kilimo cha Nyanya
Wadudu na magonjwa ni changamoto kuu.
Ni muhimu kuwa na mbinu bora za udhibiti.
Mavuno ya Nyanya kwa Ekari
Mavuno yanategemea aina ya mbegu na matunzo. Hybrid zina uwezo wa kutoa mavuno mengi zaidi.
Nyanya zinachukua siku 70 mpaka 90 kuwa tayari kuvuna tangu kupandikizwa. Nyanya zinatakiwa kuvunwa zinapokuwa zimekomaa lakini bado zikiwa na rangi ya kijani. Wakati wa kuvuna nyanya, tenganisha tunda na kikonyo chake na sio kikonyo na shina ili kuepuka kuujeruhi mmea kitu ambacho kinaweza hurahisisha maambikizi ya magonjwa kwa mimea.
Wakati mzuri wa kuvuna ni asubuhi na jioni. Inatakiwa nyanya ziwekwe kwenye vyombo vinavyopitisha hewa, na vyombo maarufu ni matenga. Matenga ya nyanya yanaweza kuwa yametengenezwa kwa mbao au mianzi. Mara tu baada ya kuvuna/kuchuma nyanya inashauriwa zikusanywe chini ya kivuli kwa muda ili ziweze kutoa joto la shambani kabla ya kuzifungasha kwenye matenga.