TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KYERWA 24-03-2025

Advertisements
PATA HABARI CHAP JIUNGE NASI WHATSAPP

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA KYERWA

Kumb. Na. FG. 740/898/11/97 24/03/2025

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa amepokea kibali cha ajira mpya kwa Ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu – Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024. Hivyo, Watanzania wote wenye sifa na uwezo wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kujaza nafasi zifuatazo:

1.0 MSAIDIZI WA MAENDELEO YA JAMII DARAJA LA II – NAFASI 06

1.1 KAZI NA MAJUKUMU

i) Kuratibu shughuli zote za Maendeleo ya Jamii kwa kuzingatia jinsia. ii) Kuraghabisha jamii kuanzia ngazi ya familia katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kusimamia, na kutathmini mipango au miradi ya maendeleo. iii) Kuhamasisha kuondokana na mila/desturi potofu na kuwa na mtazamo wa kupenda mabadiliko. iv) Kutoa taarifa za utekelezaji wa kazi zake kila mwezi. v) Kuelimisha jamii juu ya kutekeleza masuala ya kijinsia. vi) Kuhamasisha jamii kutumia teknolojia sahihi na rahisi. vii) Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutoa taarifa za matukio mbalimbali kama vifo, milipuko ya magonjwa, masoko, uzalishaji mali, vyakula, ajira, na unyanyasaji wa kijinsia. viii) Kuhamasisha jamii kujiunga na Elimu ya Watu Wazima. ix) Kuelimisha jamii kuhusu masuala ya watoto. x) Kukusanya, kuchambua, na kuweka takwimu zinazozingatia jinsia zitakazowezesha jamii kupanga mipango yao. xi) Atafanya kazi nyingine za fani yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.

1.1.1 SIFA ZA MWOMBAJI

Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo; Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

1.1.2 NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B

2.0 MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.

ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.

iii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma.

iv. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

Advertisements
JE UNA MASWALI? JIUNGE NASI WHATSAPP

v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti ya kuzaliwa, Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.

vi. “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of Results”, hati za matokeo za Kidato cha Nne na Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA, na NACTE).

viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CCA.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.

x. Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria. xi. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 05 Aprili, 2025 saa 6.00 Usiku.

xii. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:

MKURUGENZI MTENDAJI, HALMASHAURI YA WILAYA YA KYERWA, S.L.P 72, KYERWA.

xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira Recruitment Portal kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’). xiv. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Limetolewa na: MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA KYERWA

Advertisements
Join Us on WhatsApp JIUNGE NASI WHATSAPP